Yanga imekamilisha usajili wa kiungo Abdulaziz makame 'Bui' ambaye atawatumikia mabingwa hao wa kihistoria baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili
Bui kiungo wa Kimataifa wa Zanzibar ametua Yanga baada ya kuzitosa timu kadhaa zikiwemo Simba na Azam Fc
Ujio wake Yanga umemkutanisha na viungo wengine wawili kutoka visiwani Zanzibar Feisal Salum 'Fei Toto' na Mohammed Issa 'Banka' ambao wamekuwa wakifanya vizuri pamoja kwenye timu ya Taifa ya Zanzibar
Bui amefichua kuwa klabu ya Azam Fc ndio iliyokuwa na kwanza kutaka kumsajili kabla ya Simba aliyoitumikia kikosi cha vijana
Hata hivyo wakati akiwa kwenye mchakato wa kukamilisha usajili wake na Simba, Yanga iliingia kati ya kumalizana nae haraka, mwenyewe akimtaja Fei Toto kuwa alichangia kwa kiasi kikubwa kumshawishi atue Jangwani
"Timu ya kwanza kabisa kunifuata kutaka kunisajili walikuwa Azam FC, kisha Simba ambao tuliafikiana kila kitu hadi wakanitumia nauli nikamalizane nao lakini Yanga wakaingilia kati," amesema
"Nafurahi kwenda kucheza pamoja na Fei ambaye ni swahiba angu, rafiki ni kama ndugu yangu Fei Toto amechangia kwa kiasi kikubwa kunivuta Jangwani"
"Tumezoeana sana na tunajuana wapi nipo naye anajua nilipo na nini kifanyike uwanjani, siongei mengi ila kazi yangu itaongea uwanjani"
Bui anamudu vyema kucheza nafasi ya kiungo mkabaji. Ujio wake huenda ukamuondoa Fei Toto sehemu ya kiungo cha ukabaji na kumsogeza mbele zaidi kwenye majukumu ya kuchezesha timu