Salamu za shukrani za uongozi wa Yanga kwa wadau

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Jun 2019
Salamu za shukrani za uongozi wa Yanga kwa wadau

Salam za Shukrani

Uongozi wa klabu ya Yanga chini ya Mwenyekiti Dk Mshindo Msolla pamoja na kamati ya Hamasa iliyoongozwa na Mh Athony Mavunde, kwa pamoja wanatoa shukrani za dhati  kwa wanachama, mashabiki na wadau wa klabu ya Yanga kwa kufanikisha zoezi zima za uchangiaji fedha kwa ajili ya klabu ya Yanga

Aidha Dk Msolla na Mh Mavunde wanawapongeza sana wanachama, mashabiki na wadau wa Yanga wote kwa kujitoa kwa hali na mali katika michango na hatimaye kushiriki katika Tamasha la Kubwa Kuliko mwishoni mwa wiki

Pamoja na Shukrani na Pongezi hizo, Dk Msolla amewahakikishia Wanayanga wote kuwa michango yao ni ya thamani mno kwa klabu yao na kwamba uongozi utasimamia fedha hizo zitumike kwa malengo yaliyokusudiwa

Pia amewataka kuendelea kujitoa kuiunga mkono klabu yao katika vipindi vyote ili kujijengea msingi imara wa kujitegemea kupitia kwa wanachama na mashabiki wake

"Tunawashukuru sana Wanayanga wote na wadau wengine, wakiwemo wale waliotupa udhamini wakati wa tukio letu la Kubwa Kuliko maana kwa pamoja wamefanikisha azma njema iliyopangwa na kamati ya Hamasa"

"Tutawalipa kwa kuhakikisha kile walichotoa kinasimamiwa na kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa," amesema Dk Msolla

TIMU YA WANANCHI, WAWEKEZAJI NI WANANCHI

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
2h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
10h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’