Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla amemkabidhi nyaraka muhimu Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh Paul Makonda ambaye juzi kwenye Harambee ya kuichangia Yanga maarufu kama Kubwa Kuliko, aliahidi kuipa timu hiyo eneo la kujenga uwanja Kigamboni
Dk Msolla amekabidhi nyaraka hizo leo ofisi ya Mkuu wa mkoa jijini Dar es salaam mbele ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Harrison Mwakyembe
Juzi kwenye hafla hiyo Makonda alitoa ahadi hiyo baada ya Rais Mstaafu awamu ya nne Dk Jakaya Kikwete kubainisha kuwa alitoa Milioni 30 zilizonunua eneo la kiwanja cha Simba kilichopo Bunju nje kidogo ya jiji la Dar es salaam
Dk Msolla ameahidi kutumia eneo hilo kujenga shule ya kukuzia vipaji 'Academy' ya klabu ya Yanga
ADVERTISE HERE