Jana Mfanyabiashara Rostam Aziz alimpa ujumbe muhimu sana Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Kassim Majaliwa ambaye aliufikisha ujumbe huo kwa Wanayanga kwenye Harambee ya Kubwa Kuliko ambayo yeye alikuwa mgeni rasmi
Mh Majaliwa ambaye pia aliichangia Yanga Fedha Taslim Tsh Milioni 10, alisema Rostam alimuomba afikishe ujumbe wake kuwa atachangia Tsh Milioni 200
Lakini zaidi, Rostam alimwambia Waziri Mkuu awafikishie ujumbe Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla na Mwenyekiti wa Kamati ya Hamasa Mh Anthony Mavunde kuwa atahitaji kuwaona akisharejea kutoka Marekani ili awaeleze zaidi mchango wake kwa Yanga
Kwa miezi kadhaa Rostam amekuwa akihusishwa na kutaka kuwekeza kunako klabu ya Yanga
Tetesi za ujio wake Yanga zimekuwa nyingi, lakini kwa ujumbe uliotolewa na Waziri Mkuu jana, kuna jambo kubwa kati ya Yanga na Rostam Aziz litafanyika atakaporejea kutoka huko Marekani