Jana miongoni mwa mambo ya msingi aliyoyazungumza Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla kwenye hafla ya kuichangia Yanga maarufu kama Kubwa Kuliko, ni mpango wa kuwarudisha wachezaji kwenye jengo la Yanga lililoko Jangwani
Dk Msolla alisema jengo hilo lina vyumba 28 ambavyo vinaweza kutumiwa na wachezaji
Hivyo akawataka wadau kujitolea kuvifanyia ukarabati vyumba hivyo ili vianze kutumika kuelekea maandalizi ya msimu ujao

Hili ni jambo la msingi sana kwani kwa misimu kadhaa wachezaji wamekuwa wakiishi majumbani kwao huku wengine wakipangishiwa mahotelini
Wachezaji kukaa sehemu moja kuna manufaa makubwa ikiwemo kupunguza gharama
Yanga pia iko kwenye mchakato wa kukarabati uwanja wa Kaunda ambapo sehemu ya kuchezea 'pitch' itawekwa nyasi bandia ili uweze kutumika kwa ajili ya mazoezi kuanzia msimu ujao
Yanga imekuwa ikitumia gharama kubwa kukodi viwanja na gharama za malazi ya wachezaji