Mzee Kilomoni alikuwepo kuwawakilisha watani

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Jun 2019
Mzee Kilomoni alikuwepo kuwawakilisha watani

Mzee Hamisi Kilomoni kwa sasa ni maarufu sana, kwani inaelezwa ndiye mwenye Simba yake.

Michakato ya mabadiliko imekwana kuendelea baada ya yeye kutoridhia aina ya maadiliko yanayofanywa

Aidha Kilomoni anayo hati ya jengo la Simba lililopo Kariakoo.

Amegoma kuitoa kupelekea mwekezaji wa Simba Mohammed Dewji 'Mo' nae kugoma kutoa Bil 20 alizoahidi

Leo alikuwepo kwenye Kubwa Kuliko Diamond Jubilee akiwa mgeni mualikwa

Uwepo wake ni katika kuiunga mkono Yanga na Mama Fatma Karume ambaye aliwakilisha Bodi ya Wadhamini

Mama Karume amefichua kuwa jengo hilo la Simba lililopo Kariakoo, lilinunuliwa kwa fedha zilizotolewa na Marehemu Mzee Karume aliyekuwa Mwanachama wa Yanga

Hati ya jengo hilo ndio iko mikononi mwa Mzee Kilomoni...!

Hawa Simba tumewabeba kila mahali. Kwanza walitoka kwenye ubavu wa Yanga mwaka 1936, timu yao iliundwa na kundi la wachezaji waliojitenga Yanga baada ya kutokea sintofahamu

Jengo lao wanalotambia walinunuliwa na Mwanachama wa Yanga Mzee Karume!

Mzee Kikwete akawapa fedha za kununua uwanja wanaotengeneza huko Bunju!

Msemaji wao Haji Manara, amezaliwa na Sunday Manara 'Computer' mmoja wa nguli wa Yanga.

Kama alivyosema baba yake leo, Haji asitusumbue kwa sababu ni mtoto wetu, tumemzaa na tumemlea ndani ya nyumba ya Yanga!

Kweli, hawa Simba wasitusumbue kwani bila ya sisi wasingekuwepo!

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
5h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
10h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
14h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
15h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
15h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
20h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’