JK afichua aliwanunulia Simba uwanja wa Bunju

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Jun 2019
JK afichua aliwanunulia Simba uwanja wa Bunju

Rais Mstaafu Awamu ya Nne Dk Jakaya Kikwete amefichua kuwa alitoa Milioni 30 kuwapa Simba wanunue ardhi ambayo sasa wanajenga uwanja wao huko Bunju nje kidogo ya jiji la Dar es salaam

Kwa mustakabali huo Dk Kikwete amewaomba Rais Dk John Magufuli na Waziri Mkuu Mh Kassim Majaliwa aliyekuwa mgeni rasmi wa Harambee ya kuichangia Yanga, nao waichangie Yanga

Akizungumza kwenye Harambee ya Kubwa Kuliko, Dk Kikwete amesema ukiwa kiongozi unapaswa kuwa msimamizi wa timu zote na sio kutumia nafasi yako kuzionea timu nyingine

Dk Kikwete ameutaka uongozi wa Yanga kutengeneza mifumo mizuri ambayo itaiwezesha Yanga kuweza kujitegemea

Amesema haungi mkono mifumo ya uendeshaji wa timu ambao unamtegemea mtu mmoja

Hivyo utaratibu huu wa kuwashirikisha wananchi utengenezwe vizuri ili uwe na manufaa kwa timu

Aidha Dk Kikwete pia ameitaka Yanga iwekeze katika kukuza vipaji vya wachezaji wadogo

Amesema utamaduni huu wa kuwategemea wachezaji kutoka nje hauna tija kwa Taifa, wakati huo wao wakijihusisha na mpira walikuwa wakijivunia wachezaji wao wa ndani

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
19h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’