Yule Straika aliyekuwa akitajwa kumalizana na Simba, Juma Balinya amemalizana na uongozi wa Yanga leo ametambulishwa ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salam kwenye hafla ya Harambee ya kuichangia Yanga maarufu kama kubwa kuliko

Mshambuliaji huyo aliyetoka Polisi Fc ya Uganda, aliibuka kuwa mfungaji bora wa ligi kuu ya Uganda msimu uliomalizika
Mwingine aliyetambulishwa leo ni kiungo Abdul-Aziz Makame 'Bui' ambaye amekuwepo ukumbini kuwawakilisha wachezaji wengine ambao tayari wamesajiliwa


Kwa mara nyingine, Yanga imewanyan'ganya Simba wachezaji hao wawili ambao walikuwa wakiwawania
ADVERTISE HERE