Makame anaamini Stars itafanya maajabu Misri

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Jun 2019
Makame anaamini Stars itafanya maajabu Misri

Kiungo mpya wa Yanga, Abdul Aziz Makame anayetokea timu ya Mafunzo ya Zanzibar, amesema timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ itawashangaza wengi kwenye Fainali za Mataifa ya Afrika nchini Misri.

Makame amekuwa akifanya vizuri na timu ya taifa ya Zanzibar, alisema kikubwa kila mchezaji wa Stars anatakiwa kuwa na moyo wa uzalendo na kupambana.

"Ukiwa mzalendo utaweza kupigana hadi dakika za mwisho, ukiangalia timu tulizonazo kundi leti ni ngumu lakini kama kila mmoja atajitoa na kujituma basi hakuna kitakachoshindikana.

"Walicheza vizuri na Misri jana Alhamisi kikubwa ni kocha kufanyia kazi mapungufu kadhaa yaliyojitokeza ili kufanya vizuri," alisema Makame.

Alisema ndoto yake ni kuvaa jezi ya Taifa Stars kwa siku za usoni ili kutoa mchango wa kipaji chake kwa taifa.

"Naamini ni suala la muda tu kwangu kila kitu kitakaa sawa," alisema nyota huyo.

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
19h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
23h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’