Simba leo imemtambulisha Beno Kakolanya baada ya kumsajili kwa mkataba wa miaka miwili akiwa mchezaji huru
Kakolanya alifikia makubaliano ya kuvunja mkataba wake na Yanga baada ya kuondolewa kikosini na kocha Mwinyi Zahera
Mlinda lango huyo ambaye wakala wake ni Selemani Haroub mmoja wa viongozi wa Simba, aliingia kwenye mgogoro na Zahera baada ya kufanya mgomo akishinikiza alipwe madai yake
Hata baada ya changamoto hiyo kumalizwa Zahera aligoma kumrejesha kikosini akidai kutokuwa na imani nae
Mwishoni mwa mwaka jana Zahera alinukuliwa na vyombo vya habari akiutaka uongozi wa Yanga umtafutie Beno timu kwani yeye hayuko tayari kufanya nae kazi
"Nawaambia viongozi huyu mtu wamtafutie timu kabla ya dirisha la usajili kufungwa, simtaki tena ndani ya Yanga, timu zipo nyingi aende akacheze huko kwa waliokuwa wamemzuia kuja mazoezini'", alisema Zahera
"Mtu hayupo na sisi kwa muda bila sababu maalum na tulimtafuta akawa hasemi chochote sasa kwa taarifa zilizopo ni kwamba mtu anayefanya naye kazi ni kiongozi wa Simba, na kama atarudi akakaa langoni kuachia magoli itakuwaje, yeye aende tu"