Baada ya kupata nafasi ya kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika msimu ujao, Yanga na timu nyingine kutoka Tanzania zimetakiwa ziwe zimekamilisha usajili wa mashindano ya CAF ifikapo Juni 30 2019
Habari njema ni kuwa uongozi wa Yanga ulianza usajili mapema kabla taarifa ya kupata nafasi ya kushiriki michuano hiyo
Hata hivyo zoezi hilo la usajili linatarajiwa kukamilishwa kwa wakati, kocha Mwinyi Zahera ametaka kutumia michuano ya AFCON inayoanza Misri wiki ijayo kusaka wachezaji wa kuongeza nafasi za wageni zilizobaki
Inafahamika michuano ya ligi ya mabingwa ina ushindani mkali, hivyo kuna umuhimu wa kuongeza wachezaji wenye uzoefu na uwezo mkubwa
Michuano ya ligi ya mabingwa msimu huu hatua ya awali itaanza mapema kabla ya kuanza kwa ligi kuu ya Tanzania Bara msimu 2019/20
Michezo yote ya hatua ya awali itakamilika mwezi wa nane