Mchezo wa Kimataifa wa kirafiki kati ya Misri dhidi ya Tanzania umemalizika kwa wenyeji kuibuka na ushindi wa bao 1-0
Bao pekee la Misri ambayo ilitawala mchezo huo kwa muda mwingi lilifungwa na Ahmady El Mohammed kwenye dakika ya 61
Kikosi cha kocha Emmanuel Amunike kilitumia mbinu ya kujihami zaidi na kushambulia kwa kushitukiza
Huo ni mchezo wa kwanza wa kirafiki kwa kikosi cha Stars ambacho kitaumana na Senegal kwenye mchezo wa ufunguzi wa michuano ya AFCON 2019 wiki ijayo
Stars inatarajiwa kucheza mchezo mwingine wa kirafiki dhidi ya Zimbabwe kabla ya kuanza michuano hiyo




ADVERTISE HERE