Rais Mstaafu Awamu ya Nne, Dk Jakaya Mrisho Kikwete ni miongoni mwa wageni maarufu waliothibitisha kushiriki Harambee ya Kubwa Kuliko itakayofanyika keshokutwa Jumamosi Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam
Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya Uhamasishaji Dk David Luhago amesema Dk Kikwete ni miongoni mwa wageni maarufu ambao wamethibitisha kushiriki Harambee hiyo
Lugano amesema mgeni rasmi wa hafla hiyo anatarajiwa kuwa kiongozi mkubwa hapa nchini
Yanga imedhamiria kukusanya Bil 1.5 Jumamosi, ikiwa ni fedha ambazo zitakamilisha zoezi la usajili wa timu hiyo
Tiketi zimeendelea kuuzwa kupitia mitandao ya kifedha na vituo vilivyoainishwa na uongozi wa Yanga juzi Jumanne
ADVERTISE HERE