Tuje kwa wingi Kubwa Kuliko tuiwezeshe timu yetu - Mwakalebela

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Jun 2019
Tuje kwa wingi Kubwa Kuliko tuiwezeshe timu yetu - Mwakalebela

Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amewataka wadau wa klabu hiyo kujitokeza kwa wingi keshokutwa Jumamosi kwenye Harambee ya kuichangia Yanga iliyopewa jina la KUBWA KULIKO

Mwakalebela amesema msimu huu wamedhamiria kujenga kikosi imara kitakachoweza kuurejesha ubingwa wa ligi kuu pamoja na kufanya vizuri kwenye michuano ya ligi ya mabingwa

Lakini hilo litafanikiwa kama wapenzi, wanachama na mashabiki wa Yanga watajitoa kwa kununua tiketi kwa wingi na kushiriki Harambee hiyo inayosubiriwa kwa hamu

Mwakalebela amesema mchakato wa usajili bado unaendelea hata hivyo wanahitaji fedha zaidi ili kuweza kukamilisha usajili wa nyota watakaoisaidia timu hiyo kwenye ligi na michuano ya Kimataifa msimu ujao

"Tunahitaji kupata fedha ili tusajili wachezaji wazuri ambao wataitumikia kwa ushindani klabu yetu, hatutaki kuona msimu ujao tunapoteza mwelekeo, tunawaomba Wanayanga kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini kujitokeza kwa wingi au kuichangia klabu kwa njia zilizoelekezwa," amesema Mwakalebela

Inaelezwa baada ya kupata nafasi ya kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa msimu ujao, Yanga imejipanga kuongeza wachezaji wa kigeni wenye uzoefu na michuano hiyo

Kocha Mwinyi Zahera amepanga kutumia michuano ya AFCON inayoanza nchini Misri wiki ijayo kukamilisha usajili wa nyota wa kigeni

 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’