Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub "Cannavaro" na straika wa zamani wa timu hiyo, Jerry Tegete jana wamekutana na kupokeana kwa shangwe mkoani Ruvuma kisha kutoa hamasa kwa watoto.
Tegete ambaye anakipiga Majimaji kwa sasa amekutana na Cannavaro ambaye hakuwemo kwenye kikosi cha Yanga kilichotoka sare na Majimaji jana.
Nyota hao wawili wa zamani wa Taifa Stars waliungana na Mjumbe wa TFF kanda ya Njombe na Ruvuma, James Mhagama kugawa mipira 100 ambayo imetolewa na Rais wa TFF, Walace Karia.
Akizungumza katika kukabidhi mipira hiyo, Mhagama alisema anatoa mipira hiyo kama zawadi kutoka kwa Karia ili iweze kuhamasisha soka la vijana mjini hapa.

ADVERTISE HERE