Msimu huu haitakuwa kazi rahisi kwa timu zinazoshiriki ligi kuu ya Vodacom kuondoka na ushindi dhidi ya Yanga. Hilo limedhihirika kwenye michezo miwili ambayo Yanga imetokea nyuma na kupata sare ya bao 1-1.
Safu ya ulinzi ya Yanga iliyo chini ya Andrew Vicent na Kelvin Yondani inaonekana kuimarika siku hadi siku. Aidha uwepo wa Papi Kabamba Tshishimbi akiwa kiungo mkabaji umechangia kwa kiasi kikubwa utulivu wa walinzi hao wa kati.
Tshishimbi mara nyingi anafanya maamuzi sahihi hivyo kuweza kutibua mipango ya timu pinzani hata kabla hawajafika kwenye box.
Kwa mtazamo wangu, kocha George Lwandamina taratibu ameanza kuingiza filosofia yake ya soka kwenye kikosi cha Yanga ambacho kilikuwa chini ya Hans van Pluijm kabla yake.
Pluijm hupendelea kujilinda kwa kumiliki mpira zaidi wakati Lwandamina yeye hupenda kuwa na ukuta imara kisha kushambulia kwa kushitukiza.
Na ndio maana program za mazoezi za kocha Lwandamina ni ngumu zaidi. Wachezaji wa Yanga sasa wanaonekana kuwa na pumzi, stamina pengine kuliko hata wakati wa Pluijm.
Kazi kubwa iliyobaki kwa Lwandamina ni kuimarisha makali ya safu yake ya ushambuliaji ili kuzitumia vyema nafasi wanazotengeneza.
Kurejea kwa Geofrey Mwashiuya na Obrey Chirwa kwenye kikosi cha kwanza kunaonekana kuongeza kitu kwenye safu ya ushambuliaji ya Yanga.
Amissi Tambwe nae anatarajiwa kurejea kwenye mchezo dhidi ya Ndanda utakaopigwa katika dimba la Uhuru, Jumamosi ijayo.

ADVERTISE HERE