Ligi kuu ya Vodacom inaendelea tena leo mzunguuko wa tatu baada ya jana Azam FC kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar na kukwea kileleni mwa msimamo baada ya kufikisha alama saba.
Mabingwa watetezi, Yanga wako Songea kukabiliana na Majimaji katika mchezo unaotarajiwa kuwa na upinzani mkali.
Msimu uliopita Yanga ilivuna pointi zote sita kwa Maji Maji kwa ushindi wa nyumbani na ugenini, lakini kihistoria mechi za Songea huwa ni ngumu kwa Yanga hata iwe na kikosi bora kiasi gani.
Mechi nyingine za Ligi kuu zinazopigwa leo Mbao watakuwa wageni wa Mtibwa Sugar Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro.
Tanzania Prisons watakuwa wenyeji wa Ndanda FC saa 10: 00 jioni kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya, Lipuli FC watakuwa wenyeji wa Ruvu Shooting Uwanja wa Samora, Iringa wakati Stand United wataikaribisha Singida United Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.
Ligi Kuu itaendelea tena kesho Uwanja wa Sokoine, Mbeya City wakiikaribisha Njombe Mji na Uwanja wa Uhuru, Simba SC wakiikaribisha Mwadui FC ya Shinyanga mechi zote zikianza Saa 10: 00 jioni.

ADVERTISE HERE