Msimu wa kwanza wa kocha Mwinyi Zahera kwenye kikosi cha Yanga umekuwa na mafanikio licha ya timu kutotwaa taji lolote
Kumaliza katika nafasi ya pili ligi kuu ya Tanzania Bara ni mafanikio kwa Zahera kwani kwa hali iliyokuwa nayo Yanga, kama angekuwa kocha mwingine pengine timu ingekuwa inapambana isiteremke daraja
Kabla ya kuja Zahera, Yanga ilikuwa na kocha George Lwandamina ambaye alivumilia changamoto zilizopo lakini baadae akashindwa akaikacha timu licha ya kuisaidia kutinga hatua ya makundi kombe la Shirikisho Barani Afrika yeye akirudi zake Zambia kuungana na timu yake ya zamani, ZESCO United
Zahera aliichukua Yanga iliyokuwa haina matumaini, kila mdau alikuwa amekata tamaa
Timu haikuwa na uwezo wa kufanya usajili wa maana huku pia ikishindwa kulipa mishahara ya wachezaji hali iliyopelekea migomo
Mcongomani huyo akaja na wazo la kuwashirikisha Wanayanga kuichangia timu yao ili kuweza kuiondoa kwenye changamoto inazokabiliana nazo

Alipendekeza kila Mwanayanga kuichangia timu angalau Tsh 2500/- kwa mwezi ambapo makadirio ya fedha ambazo zingekusanywa zingefikia zaidi Tsh Bilioni 12
Kwa ushirikiano na viongozi waliopita na waliopo, wazo hilo liliboreshwa kwa kuundwa Kamati Maalum ya Hamasa na hatimae leo Wanayanga wanaona fahari kuichangia timu yao
Aidha matunda ya kampeni hiyo yanaonekana sasa kwenye usajili ambapo Yanga imeweza kusajili wachezaji inayowataka
Tayari hofu imetanda upande wa pili kwani hiki kinachofanywa na Yanga kwenye dirisha la usajili hawakukitarajia
Sasa hivi huwasikii tena wakibeza 'bakuli' la Yanga kwani limeanza kulipa
cutAidha, Juni 15 Yanga imeandaa Harambee kubwa zaidi iliyopewa jina la KUBWA KULIKO ambapo wadau wa timu hiyo wanaendelea kununua tiketi kuweza kuwa sehemu ya Historia itakayo andikwa ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam
Kupitia Harambee hiyo, Yanga imejipanga kukusanya fedha kuongeza nguvu katika michakato ya usajili inayoendelea bila ya kusahau kupata fedha za kutosha kwa ajili ya kulipa mishahara ya wachezaji msimu mzima
Ndio! Yanga imejipanga kuwa na fedha kwa ajili ya kulipa wachezaji wake msimu mzima na hivyo kufanya mchakato wa mabadiliko bila ya kuwa na 'presha' tofauti na ilivyokuwa kwa watani zao Simba ambao waliikabidhi timu kwa mwekezaji kwa Bilioni 20 tu
Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Yanga zimebainisha kuwa thamani ya Yanga ni Bilioni 120 hivyo wakati mchakato wa mabadiliko utakapoanza, mwekezaji anapaswa kuwa na angalau na kiasi hicho cha pesa
Hapo ndipo itazaliwa Yanga ya Kimataifa!