Beki wa kushoto wa Yanga Gadiel Michael amepona majeraha ya kifundo cha mguu yaliyomuweka nje kwa takribani mwezi mzima
Gadiel aliitwa kikosi cha Stars cha kocha Emmanuel Amunike ambacho tayari kimeingia kambini kujiandaa na AFCON 2019
Beki huyo mahiri wa kupiga krosi tayari ameripoti kambi ya Stars
Gadiel ni miongoni mwa wachezaji ambao wamemaliza mikataba Yanga na mazungumzo ya mkataba mpya bado yanaendelea
Huenda msimu ujao akachuana vikali kuwania namba na beki mwenye kasi Erick Rutanga ambaye inaelezwa tayari amesajiliwa na Yanga kutoka klabu ya Rayon Sports
ADVERTISE HERE