Stars yafanya maandalizi ya AFCON uwanja wa Taifa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Jun 2019
Stars yafanya maandalizi ya AFCON uwanja wa Taifa

Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kiliingia kambini juzi kujiandaa na michuano ya AFCON 2019 itakayofanyika Misri kuanzia Juni 21 2019

Stars iliyoweka kambi Hoteli ya Whitesands, inafanya mazoezi kwenye uwanja wa Taifa ambapo baadhi ya wachezaji walianza mazoezi jana

Baadhi ya nyota wa timu hiyo jana walishiriki kwenye mchezo wa hisani kati ya Marafiki wa Mbwana Samatta na Marafiki wa Ali Kiba mchezo uliopigwa uwanja wa Taifa na Marafiki wa Samatta kuibuka na ushindi wa mabao 6-3

Wachezaji wote 39 walioteuliwa na kocha Emmanuel Amunike wanashiriki kwenye mazoezi hayo mpaka Juni 07 ambapo wachezaji saba watachujwa tayari kwa safari ya kuelekea nchini Misri

Juni 13 Stars itajipima katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Misri, wenyeji wa michuano hiyo

Mechi ya kwanza ya Stars itapigwa Juni 23 dhidi ya Senegal, moja ya timu zinazopewa nafasi ya kufanya vizuri kwenye michuano hiyo

Kikosi cha Senegal kitaongozwa na mshambuliaji wa Liverpool Sadio Mane ambaye aliibuka mfungaji bora wa ligi kuu ya Uingereza sambamba na Pierre Emerick Aubemeyang na Mohammed Salah

cut

Mbali na Senegal, Stars iko kundi C na timu za Algeria na Kenya

Ili kuweza kufanya vizuri katika kundi hili, Stars inahitaji kufanya maandalizi kabambe kwani ukiondoa Kenya, Senegal na Algeria ni timu ambazo zimekamilika zikiwa na nyota wengi wanaosakata kabumbu barani Ulaya

Tanzania inachukuliwa kama 'under-dog' wa kundi hili

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
32m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
18h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
22h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
23h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
23h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’