Nahodha wa Simba John Bocco anatajwa kuwa mfungaji bora wa muda wote ligi kuu ya Tanzania Bara akiwa amefunga mabao 114 tangu alipoanza kuitumikia Azam Fc kwenye ligi hiyo mwaka 2008
Hata hivyo ni kama Bocco anapewa sifa asiyostahili kwani mkongwe, legendari wa Yanga Mohammed Hussein Mmachinga (pichani juu, wa pili kutoka kushoto waliochuchumaa) takwimu zinaonyesha amefunga mabao zaidi ya 150
Kulingana na takwimu zilizotolewa na Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten ambazo zimethibitishwa na Mmachinga mwenyewe, amefunga mabao 152
TAKWIMU ZA MOHAMEDI HUSSEIN 'MMACHINGA'
1. 1993 magoli 13
2. 1994 magoli 20
3. 1995 Magoli 21
4. 1996 magoli 14
5. 1997 magoli 12
6. 1998 magoli 26
7. 1999 magoli 11
8. 2000 magoli 13
9. 2001 magoli 4
10.2002 magoli 3
11. 2003 magoli 5
12.2004 magoli 4
13. 2005 magoli 7
Mmachinga alifunga mabao hayo wakati akicheza katika timu za Bandari Mtwara,Yanga SC, Simba SC, Mbanga Fc Kigoma, Twiga Kinondoni