Katibu Mkuu wa Yanga Charles Boniface Mkwassa amewataka mashabiki wa timu hiyo wasitaharuki mpaka kuharibu mali kwa tukio la Haruna Niyonzima kuondoka Yanga.
Mkwassa ameyasema hayo leo alipozungumza na waandishi wa habari.
Amesema ni jambo la kawaida kwa wachezaji kuhama kutoka timu moja kwenda nyingine wala hakuna sababu ya baadhi ya mashabiki kuchoma jezi zenye jina la Haruna Niyonzima.
"Siungi mkono tabia hiyo na haipendezi machoni mwa watu. Ni kawaida kwa mchezaji kutoka timu moja kwenda nyingine hakuna sababu kwa mashabiki kufanya matukio ya aina hiyo kwani wanaidhalilisha klabu pia."
Yanga imeachana na Niyonzima aliyeitumikia kwa miaka sita baada ya mchezaji huyo kudai dau kubwa la usajili.
Inadaiwa kuwa Niyonzima alitaka kupewa Tsh Mil 130 yote kwa mkupuo wakati Yanga ilikuwa tayari kutoa Mil 85 huku ikiahidi kumalizia nyingine baadae.
Baada ya mchezaji huyo kugomea mpango huo ndipo viongozi wa Yanga walipofikia makubaliano ya kuachana nae.

ADVERTISE HERE