Wakati ulipotangazwa mchakato wa kuichangia Yanga ili iweze kuboresha kikosi chake, wapo waliobeza wakiamini jambo hilo haliwezi kufanikiwa
Lakini kwa michakato ya usajili inayoendelea huko Jangwani, ni wazi zoezi hilo linaelekea kufanikiwa japo uongozi wa Yanga kupitia Kamati yake ya Hamasa bado haujaweka hadharani kiasi cha fedha zilizokusanywa
Kwa hatua hii, Wanayanga wote wanaoshiriki zoezi la kuichangia timu wanastahili pongezi na wanapaswa kuendelea kuchangia kwani imedhihirika kuwa kumbe wanaweza kuisimamia timu wao wenyewe wakati uongozi ukijipanga kubadili mfumo wa uendeshaji
Aidha kocha Mwinyi Zahera nae anastahili pongezi kwa kuja na wazo hili ambalo baada ya kuwekewa mkazo limeanza kuleta matumaini
Mafanikio itakayopata Yanga msimu ujao yatawaweka kifua mbele wadau wake kwani wameshiriki kikamilifu kuirudisha timu hiyo katika hali ya ushindani
cutJuni 15 2019 kutakuwa na tukio kubwa la Harambee ya kuichangia Yanga 'KUBWA KULIKO' ambalo litafanyika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam
Wanayanga wameaswa kushiriki tukio hilo kwa kununua tiketi mapema kwani siku hiyo Yanga itaandika historia na kudhihirisha ule msemo usemao UMOJA NI NGUVU, UTENGANO NI UDHAIFU
Wiki iliyopita Katibu wa Kamati ya Hamasa Deo Mutta alifafanua kuwa fedha zinazochangishwa sasa hazitatumika kwa usajili pekee, bali zitalipa madeni ya wachezaji waliopo pamoja na kulipa mishahara ya wachezaji angalau kwa msimu wote ujao wakati Yanga ikijipanga kufanya mabadiliko
Inafahamika, moja ya changamoto iliyoikwamisha Yanga msimu uliomalizika ni 'ukata' uliopelekea kucheleweshwa kwa mishahara ya wachezaji.
Lakini kama timu itakuwa na uhakika wa kuwalipa wachezaji wake kwa mwaka mzima, basi itakuwa na wasaa wa kujikita zaidi katika kufanya mambo mengine muhimu ya manufaa kwa timu
Wakati watani zao Simba wakitamba kuwa na fedha baada ya kubadili mfumo wa uendeshaji, lakini kiuhalisia bado timu hiyo inamtegemea mtu mmoja 'Mo' ambaye ndiye mwekezaji huku ikielezwa mpaka sasa zile Bilioni 20 za kununua hisa asilimia 49 bado hajazitoa
Kwa umoja huu wa wadau, Yanga inaweza kukusanya fedha nyingi na kuzima tambo za wapinzani wao kupitia usajili uanoendelea sasa
Licha ya umasikini wao, 'nguvu ya buku' ya Wanajangwani imeanza kuonyesha makali