Kiungo Mafunzo ambaye yuko kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Zanzibar, Abdulaziz Makame, amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Yanga
Makame anakuwa mchezaji wa kwanza wa ndani kusajiliwa na Yanga msimu huu

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23 alikuwa akiwaniwa na timu za AFC Leopards ya Kenya na Simba ya jijini Dar es salaam lakini ni Yanga iliyofanikiwa kuipata sahihi yake
Inaelezwa Simba ilimtumia Makame tiketi ya Boti kuja jijini Dar lakini Yanga ikatuma tiketi ya Ndege na kuwapiga chenga mabosi wa Simba waliokuwa wakimsubiri Bandarini
Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera ameidhinisha usajili wa Makame ambaye atakuwa miongoni mwa wachezaji wanne wazawa wakaosajiliwa na Yanga
ADVERTISE HERE