Lwandamina asaka tiba ya mabao

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
15 Sep 2017
Lwandamina asaka tiba ya mabao
Yanga bado haijawa na kasi nzuri katika kupachika mabao, jambo ambalo limemgusa kocha George Lwandamina, ambaye juzi alitumia muda mwingi wa mazoezi yake kufanyia kazi umaliziaji.

Yanga iliyofunga mabao 57 msimu uliopita, msimu huu imeanza kwa kasi ndogo ikifunga mabao mawili tu katika mechi mbili za awali, jambo ambalo limemtikisa Lwandamina.

Kocha huyo wa zamani wa timu ya Taifa ya Zambia, amewataka wachezaji wake wote kujenga uwezo wa kupiga mashuti na kumalizia nafasi kwa kasi ili timu yao ipate matokeo bora.

Katika mazoezi hayo, kazi ya kupiga mashuti ilifanywa na wachezaji wote na siyo mastraika pekee.

Akizungumza punde baada ya mazoezi hayo, Lwandamina alisema anataka kwenye kikosi chake kila mchezaji awe na uwezo wa kupachika mabao, lakini wanatakiwa kufanya kazi hiyo kwa kasi ya ajabu.

“Tunataka kila mchezaji ajenge uwezo wa kufunga, kwa kuwa kuna wakati timu inapanda kushambulia na hata mabeki nao huenda kusaidia, akipata nafasi afunge,” alisema Lwandamina.

“Tuna changamoto katika eneo la kufunga na kulimaliza, hivyo ni lazima kuwapa wachezaji uzoefu kwenye kufunga, hilo litakuwa msaada zaidi kwetu.

“Tukiwa vizuri kwenye kufunga timu itafanya vizuri zaidi, japo hili halijengwi kwa siku moja, linakwenda taratibu hadi wachezaji watakapozoea.”

Akiwazungumzia washambuliaji wake, kocha huyo alisema wanatakiwa kujenga hali ya kujiamini zaidi na kupambana kwa dakika zote uwanjani ili kufanya vizuri. “Kuwa shujaa ni lazima ujitoe, upambane kwa muda mwingi na kuhakikisha kuwa unafunga,” aliongeza.

“Straika hatakiwi kuwa mwoga kwa mabeki, anatakiwa kuwaza kufunga tu kila anapoona nafasi.”

Katika hatua nyingine, Lwandamina ameshangazwa na kitendo cha Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) pamoja na Bodi ya Ligi kutoa ratiba ambayo haina mapumziko.

Lwandamina alisema ni ajabu kwa mechi kuchezwa msimu mzima bila ya kuwa na wakati wa kupumzika.

“Itakuwa ni jambo gumu kwetu, hata kama una wachezaji makini, ni ngumu kucheza msimu mzima bila kupumzika,” alisema.

Kwa hisani ya MCL
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE →
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE →
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11h ago
READ MORE →
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE →
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
15h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE →
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE →
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE →
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE →