Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera jana usiku alikamilisha usajili wa wachezaji wanne kabla ya kuondoka kuelekea DR Congo anakokabiliwa na majukumu ya timu ya Taifa
Aidha Mcongomani huyo alisema wachezaji 11 watasaini mikataba ya kuitumikia Yanga leo na kesho
Miongoni mwa wachezaji hao nane ni wa kigeni na watatu ni wazawa
"Nikitoka hapa nakwenda kusajili wachezaji wanne kabla sijaondoka saa nane usiku kwenda Congo. Wengine watatu watasaini kesho" Zahera aliwaambia waandishi wa habari jana kwenye Mkutano baada ya mchezo dhidi ya Azam Fc
"Tutasajili wachezaji nane wa kigeni, wengine wanatarajiwa kusaini katika kipindi cha siku mbili"
"Kwa wale wa hapa Tanzania nimeacha maelekezo nani asajiliwe, hivyo watasaini bila ya mimi kuwepo"
cutKuhusu wachezaji wanaoachwa Zahera amesema ana wachezaji 19 waliomaliza mikataba
"Wachezaji 19 wamemaliza mikataba nitaangalia, naweza kuacha wote nikasajili wengine...!"
Taarifa za wachezaji waliosajiliwa zitatolewa na uongozi wa Yanga baada ya michakato yote kukamilika