Ajib amechezea bahati - Zahera

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 May 2019
Ajib amechezea bahati - Zahera

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema kiungo Ibrahim Ajib amepoteza bahati ya kujiunga na TP Mazembe, timu ambayo ingemlipa vizuri pamoja na kuboresha kiwango chake

Aidha Zahera amesema hafahamu alipo Ajib kwa sasa, mara ya mwisho uongozi wa Yanga ulimtaarifu kuwa anaumwa na hakucheza michezo miwili iliyopita

"Mimi nilimwambia Ajibu, kocha wa TP Mazembe alinipigia simu kaniuliza kuhusu weweΒ  nimeshampa habari zako, wewe unasemaje? akaniambia napenda kwenda nje, nipo tayari kwenda Mazembe," alisema Zahera

"Baada ya siku kadhaa Mazembe wakatuma barua kumtaka Ajibu, kuanzia hapo mimi sijui chochote wala alipo Ajibu. Niliambiwa anaumwa Malaria hata mechi mbili zilizopita hakucheza."

"Mambo mengine sijui kama alisaini Ndanda, Lipuli au Mazembe. Nasikia tu wanasema Ajibu hataenda tena Mazembe anaenda Simba mara anabaki Yanga"

Zahera amesema ni nadra sana kwa mchezaji kupata nafasi ya kutakiwa na vilabu vikubwa kama TP Mazembe, Al Ahly nk

Amesema TP Mazembe ni klabu inayolipa wachezaji vizuri lakini pia ni timu inayotunza wachezaji vyema kwa kuwa imejitosheleza. Ina vifaa ambavyo hata baadhi ya timu Ulaya hazina

cut

"Mchezaji kama Ajibu, Simba na Yanga haziwezi kumlipa kama ambavyo angelipwa na TP Mazembe," amesema

"Ukiachana na pesa, Mazembe ni klabu inayotunza vizuri wachezaji wake, inawezekana hata baadhi ya vilabu vya Ulaya havifanyi hivyo. Kuna wakati nilikuwa Lubumbashi na timu ya taifa, niliangalia mambo ya Mazembe nikabaki mdomo wazi"

"Sasa kama hupendi kwenda Mazembe, hivi vilabu viwili vya Simba na Yanga hawezi kukupa pesa zaidi ya Mazembe"

"Kwangu nadhani kakataa kwa sababu moja, labda anaona hapa kila siku anaandikwa kwenye magazeti yote, akipita mitaani watu wanamwita na kumsifia lakini kule mambo hayo hayatakuwepo kunama-star wengi."

"Au anaogopa akienda kule hatocheza, kama amekataa kwenda ili abaki hapa sawa lakini mimi hawezi kunidanganya, Mazembe wataniambia kilakitu."

"Sio kila siku utapata fursa ya kuitwa na klabu ya hadhi ya TP Mazembe, Al Ahly au timu nyingine kubwa za Afrika"

Ajib atakosa mchezo wa mwisho wa Yanga ambapo leo inashuka uwanja wa Uhuru kumenyana na Azam Fc

Pengine mashabiki wa Yanga hawatamuona tena kiungo huyo kinara wa pasi za mabao akiwa ndani ya uzi wa mabingwa hao wa kihistoria kwani kuna kila dalili kwa yeye kujiunga na watani zao Simba

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
6h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
21h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’