Yondani amtibua Zahera

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 May 2019
Yondani amtibua Zahera

Kikosi cha Yanga leo kimeendelea na mazoezi kwenye uwanja wa Chuo cha Polisi Kurasini jijini Dar es salaam kujiandaa na mchezo wa mwisho wa ligi kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Azam Fc utakaopigwa Jumanne, May 28 dimba la Uhuru

Kocha Mkuu wa mabingwa hao wa kihistoria Mwinyi Zahera amesema baadhi ya wachezaji waliokuwa wagonjwa wameanza kurejea kikosini

"Paul Godfrey alikuwa mgonjwa lakini leo ameanza mazoezi. Dante, Abdul, Ngasa, Banka, Jaffar na Ajib bado wagonjwa," amesema

Katika hatua nyingine Zahera amemuagiza Meneja wa Yanga Nadir Haroub kumsaka beki wa timu hiyo Kelvin Yondani ambaye haonekani mazoezini

Zahera amesema hana taarifa kama Yondani ni mgonjwa, amejaribu kumpigia simu bila ya mafanikio

"Sina taarifa za Yondani, nimejaribu kumpigia simu lakini hapokei, tumemtuma Meneja (Nadir) aende akamtafute kwake anipe mrejesho kabla sijafanya maamuzi," Zahera aliiambia eFM

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
4h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
8h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
12h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
13h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’