Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera tayari ameaga kuwa wiki ijayo baada ya mchezo wa mwisho wa kumaliza msimu dhidi ya Azam Fc May 28, ataondoka kuelekea kwao DR Congo kuungana na timu ya Taifa inayotarajiwa kuweka kambi nchini Hispania
Hata hivyo Zahera amefichua kuwa atakamilisha usajili wa wachezaji wapya nane, na kabla hajaondoka, ataweka kila kitu hadharani
Miongoni mwa wachezaji hao, inaelezwa sita ni wa kigeni na wawili ni wazawa
Aidha, baada ya mchezo huo pia Zahera ataweka hadharani majina ya wachezaji walioachwa na timu hiyo
"Kila kitu kimekamilika, subiri baada ya mchezo wetu na Azam Fc, nitawataja wachezaji niliowasajili na wachezaji ambao tumewaacha," amesema
cutAjib na Makambo hawamuumizi kichwa
Jana baada ya mchezo dhidi ya Mbeya City, Zahera alithibitisha kuwa kiungo wake Ibrahim Ajib atasajiliwa na TP Mazembe
Lakini akawatoa hofu mashabiki wa Yanga kuwa kuondoka kwa kiungo huyo kutatoa nafasi kwa wachezaji wengine wazuri kusajiliwa Yanga
"Sina wasiwasi wowote sababu kama Ajib ataondoka basi Ajib mwingine anakuja," alisema Zahera
Kauli kama hiyo aliitoa aliporejea kutoka Guinea alikokwenda kusimamia mazungumzo ya mauzo ya Heritier Makambo kwenda klabu ya Horoya AC
"Nawaambia mashabiki wa Yanga wasiwe na wasiwasi, tutasajili mshambuliaji hatari zaidi ya Makambo"