Klabu ya Yanga tayari imesaini mkataba na televisheni ya Azam kwa ajili ya kurusha kipindi cha klabu ya Yanga (Yanga TV) kinachotarajiwa kuanza kuonekana hivi karibuni.
Kulingana na Mkuu wa Kitengo cha Habari cha Yanga, Dismas Ten, tayari mkataba baina ya Yanga na Azam umeshasainiwa amapo kwenye mkataba huo Yanga itavuna kiasi cha Mil 100 kwa mwaka.
Aidha Ten amesema kupitia kipindi hicho Yanga itakusanya mapato zaidi kupitia matangazo ya wadhamini wengine.
Utaratibu huu utawezesha na pengine kuondoa kabisa utegemezi wa klabu kwa watu binafsi.
Ikumbukwe tayari Yanga imeandaa utaratibu wa kuongeza mapato kupitia vifaa vyake vya michezo ambapo bidhaa hizo zitauzwa kwenye mtandao wa klabu ya Yanga unaotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni.
Bidhaa hizo pia zitauzwa kwenye maduka kote nchini, kupitia maduka rasmi yatakayotangazwa na klabu.

ADVERTISE HERE