Haji Mwinyi ajiandaa na maisha nje ya Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 May 2019
Haji Mwinyi ajiandaa na maisha nje ya Yanga

Beki Haji Mwinyi ni miongoni mwa wachezaji wa Yanga ambao mikataba yao inamalizika baada ya mchezo wa mwisho wa ligi

Beki huyo aliyeitumikia Yanga kwa zaidi ya miaka minne, atakuwa huru baada ya Yanga kuumana na Azam Fc wiki ijayo

Amezikaribisha timu zinazohitaji huduma yake kwa ajili ya msimu ujao

"Mkataba wangu na Yanga unamalizika msimu huu. Baada ya hapo nitakuwa huru"

"Nakaribisha klabu yeyote inayohitaji huduma yangu kwa msimu ujao waje tukae mezani tuzungumze, lakini kuhusiana na ofa nilizonazo mezani hadi sasa siwezi kuweka wazi hadi hapo nitakapomaliza msimu wangu kwa michezo miwili iliyobaki," Mwinyi aliiambia Mwanaspoti

"Sikuwa na namba kikosi cha kwanza, lakini hiyo haina maana kwamba kiwango changu kimeshuka, nipo vizuri na nina uwezo wa kupambana. Kutokana na uzoefu nilionao na naweza kucheza timu yeyote"

Haji Mwinyi hakuwa na wakati mzuri msimu huu katika kikosi cha Zahera akishindwa kutamba mbele ya Gadiel Michael aliyekuwa chaguo la kwanza

Yanga imepanga kutowaongezea mikataba wachezaji ambao hawakucheza angalau nusu ya michezo ya ligi kuu msimu huu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’