Wachezaji saba Yanga wagonjwa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 May 2019
Wachezaji saba Yanga wagonjwa

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema wachezaji saba wa kikosi cha Yanga hawataweza kucheza kesho mchezo dhidi ya Mbeya City baada ya kukumbwa na Malaria

Wachezaji hao ambao hawakufika kufanya mazoezi yaliyofanyika uwanja wa Uhuru leo ni pamoja na Abdallah Shaibu, Andrew Vicent, Juma Abdul, Ibrahim Ajib, Said Makapu, Mohammed Issa na Paulo Godfrey

"Nadhani timu yetu imekumbwa na janga la Malaria, tuna wachezaji karibu saba ambao wanaugua Malari," amesema Zahera

"Sijui ni kama walikula nini sijui"

Akizungumzia mchezo wa kesho, Zahera amesema hautakuwa mwepesi kutokana na ubora wa kikosi cha Mbeya City

"Tuliwafunga mchezo wa kwanza, lakini wachezaji ilibidi wajitume sana kuweza kupata matokeo," amesema

"Kesho pia mchezo hautakuwa tofauti lakini nafurahi wachezaji wangu wamepata muda mrefu wa kupumzika hivyo watakuwa 'fresh'"

"Kwa wale watakaocheza lengo letu ni moja, tumalize mechi mbili zilizobaki kwa kuibuka na ushindi"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
8m ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
20h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’