Kikosi cha Taifa Stars kinatarajiwa kuondoka leo jioni nchini kuelekea Afrika Kusini kwa ajili ya kushiriki michuano ya COSAFA itakayotimua vumbi Juni 25 mwaka huu huku wakijiamini kufanya vizuri.
Akizungumza na vyombo vya habari Jijini Dar es Salaam leo, kocha wa Mkuu Salum Mayanga amesema kikosi chake kipo katika hali nzuri kiafya hivyo wanatarajia kufanya vyema katika mashindano hayo.
"Vijana wote wapo sawa tayari kwa michuano ya COSAFA, tunaimani tutafanya vyema. Watanzania watupe sapoti" alisema Mayanga.
Naye Nahodha msaidizi wa kikosi hicho Himid Mao amesema wachezaji wenzake wamejiandaa vizuri katika kutafuta ushindi wa michuano hiyo ili waweze kuendelea mbele katika hatua nyingine.
Taifa Stars imepangwa kundi A ambako wapinzani wake ni Mauritius, Malawi na Angola wakati Kundi B ni Msumbiji, Shelisheli, Madagascar na Zimbabwe.

ADVERTISE HERE