Ukiachana na kutangaza kuajiri kocha Msaidizi mzawa, Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla amepanga kuifanyia marekebisho safu yote ya uongozi klabuni hapo
Dk Msolla ameagiza waajiliwa wote wa Yanga kuwasilisha taarifa zao za elimu na nakala za vyeti ili kuhakikisha watu sahihi wanafanya kazi wanazostahili
Kocha huyo wa zamani wa timu ya Taifa, amesema tangu aanze majukumu yake Yanga amebaini kuwepo kwa baadhi ya Wafanyakazi ambao watakeleza majukumu yasiyo yao huku wengine wakikosa sifa za kutumikia nafasi zao
"Tunataka kila mtu afanye kazi anayostahili, naamini mabadiliko haya tunayotaka kufanya, yataongeza ufanisi katika utendaji wa Wafanyakazi wetu," amesema Dk Msolla
ADVERTISE HERE