Yanga kuunda Kamati ya Usajili

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 May 2019
Yanga kuunda Kamati ya Usajili

Uongozi wa klabu ya Yanga uko katika mchakato wa kuunda Kamati ya usajili ambayo itashirikiana na Kocha Mwinyi Zahera kusimamia usajili wa timu hiyo

Akizungumza na waandishi wa habari leo katika Mkutano uliofanyika Makao Makuu ya Yanga jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa timu hiyo Dk Mshindo Msolla amesema tayari uteuzi umeshafanyika kwa sasa wanafanya majadiliano na wajumbe walioteuliwa kabla ya kuwaweka hadharani

"Wajumbe wa Kamati hiyo tumeshawateua lakini hatuwezi kuwatangaza kabla nao hawajaridhia," amesema Dk Msolla

"Wiki ijayo tutakuwa na kikao na benchi la Ufundi, pengine katika kikao hicho tutaitangaza Kamati"

"Msimu huu tumedhamiria kufanya usajili makini wenye tija"

Aidha Dk Msolla amesema hata hivyo jukumu la kutafuta wachezaji litabaki kwa kocha Zahera na benchi lake la ufundi, Kamati hiyo itakuwa na jukumu la kumsaidia kukamilisha michakato ya usajili baada ya makubaliano kufikiwa

Dk Msolla amesema kuanzia msimu ujao watawatumia wachezaji waliocheza Yanga zamani kutafuta wachezaji

"Msimu ujao kazi kubwa itafanywa na wachezaji wetu wa zamani kwani tutawapa jukumu la kutembea mikoani kutafuta wachezaji wenye vipaji"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’