Mabingwa wa kihistoria Tanzania, Yanga leo wanashuka kunako uwanja wa Uhuru kuikabili Ruvu Shooting katika mchezo wa raundi ya 36, ligi kuu ya Tanzania Bara
Baada ya Simba kulazimishwa suluhu ya bila kufungana na Azam Fc jana, matokeo hayo yametoa mwanya kwa Yanga kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi kama itapata ushindi leo
Vijana wa Mwinyi Zahera bado hawajakata tamaa katika kuwania ubingwa wakihitaji kushinda michezo mitatu iliyobaki
Yanga inaweza kufikisha alama 89 na ili waondolewe katika mbio za ubingwa Simba inapaswa kushinda angalau michezo mitatu kati ya mitano iliyobaki
Baada ya mchezo wa leo, Yanga itashuka tena dimba la Uhuru May 22 kuikabili Mbeya City na kumaliza msimu kwa kucheza na Azam Fc May 26
ADVERTISE HERE