Tambwe asubiri mkataba mpya Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 May 2019
Tambwe asubiri mkataba mpya Yanga

Mkataba wa mshambuliaji Amissi Tambwe unamalizika mwishoni mwa msimu.

Hata hivyo bado hakuna mazungumzo ya mkataba mpya yaliyoanza baina yake na uongozi wa Yanga

Tambwe aliyetua Yanga mwaka 2014 akitokea Simba wakati wa usajili wa dirisha dogo, anaamini bado anaweza kuisaidia Yanga

Tambwe anashikilia rekodi ya kupachika mabao 72 kwenye ligi kuu tangu atue nchini, amesema anausikiliza uongozi wa timu hiyo

"Bado napenda kuendelea kucheza Yanga, hivyo nawasikiliza viongozi kama wataniongezea mkataba. Lakini hata kama hawataniongeza, nitaendelea na maisha ya soka sehemu nyingine," amesema

Msimu uliopita haukuwa mzuri kwa Tambwe kwani alikuwa nje kwa muda mrefu akisumbuliwa na majeraha ya goti

Kwa kiasi kikubwa, majeraha hayo yalipunguza kasi yake ya kupachika mabao, msimu huu akiwa amefunga mabao nane tu

Hata hivyo Tambwe amesema kwa sasa amepona kabisa majeraha na anaamini kama angepata nafasi kubwa ya kucheza, angefunga mabao mengi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’