Msimu ujao zamu yetu - Dk Msolla

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 May 2019
Msimu ujao zamu yetu - Dk Msolla

Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Dk Mshindo Msolla amewaahidi mashabiki wa timu hiyo kuwa msimu ujao utakuwa wa furaha kwao

Msolla aliyechaguliwa kwa kishindo wiki iliyopita, ameahidi kuirudisha Yanga katika anga za Kimataifa, kazi hiyo uongozi mpya tayari umeianza

Tangu kuondoka wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Yanga Yusufu Manji, timu imeshindwa kusimama kutokana na kukumbwa na changamoto za kiuchumi

"Nafahamu kwamba mashabiki wa Yanga wamekosa furaha kwa muda mrefu, lakini nawaahidi kuanzia msimu ujao furaha itarejea tena kama zamani," amesema

"Baada ya msimu huu kumalizika, tutaiunda upya timu yetu kwa kushirikiana na kocha Mwinyi Zahera. Lazima tuunde timu imara ambayo itawafanya Wanayanga watembee kifua mbele"

Dk Msolla ameahidi kurudisha utaratibu wa enzi ya Manji ambapo timu hiyo ilikuwa ikienda kuweka kambi nje ya nchi, upo uwezekano wa mabingwa hao wa kihistoria kwenda kuweka kambi Ulaya kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao

Aidha mabadiliko ya mfumo ya uendeshaji ni kipaumbele cha kwanza cha Dk Msolla na timu yake baada ya kipindi hiki cha mpito

"Nina mipango endelevu ya kuifanya klabu kujiendesha kibiashara na kuwa klabu tajiri"

"Hii ni timu kongwe tangu mwaka 1935, lakini imeshindwa kujikomboa kiuchumi na kutegemea wafadhili katika kujiendesha, hivyo siko tayari kuona hilo na nitahakikisha naacha alama," amesema

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
3h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
19h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’