Tutamwaga fedha kuifumua Yanga - Msolla

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 May 2019
Tutamwaga fedha kuifumua Yanga - Msolla

Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla amesema kikosi cha timu hiyo kinahitaji mabadiliko makubwa na wamejipanga kuyafanya

Baada ya kuondoshwa kwenye michuano ya kombe la FA kwa kufungwa mabao 2-0 na Lipuli Fc katika mchezo wa nusu fainali, Yanga ina matumaini madogo ya kushiriki michuano ya CAF msimu ujao, kwani nafasi pekee iliyobaki ni ya kushinda taji la ligi kuu

Hata hivyo nafasi ya kutwaa taji la ligi kuu ni ndogo sana kwani itategemea na wapinzani wao Simba wanaongoza ligi kufanya makosa katika michezo iliyobaki huku Yanga ikihitaji kushinda michezo yote

Dk Msolla aliyechaguliwa mwishoni mwa wiki kuiongoza Yanga, amesema wanafahamu wana kazi kubwa ya kufanya kuirejesha Yanga katika ubora wake

"Nilizungumza na kocha hata kabla sijachaguliwa kuiongoza Yanga, aliniambia wachezaji ambao anadhani wanastahili kuendelea kubaki Yanga hawazidi 10"

"Yeye alihitaji tumpatie Bil 1.5 ili aweze kufanya usajili, lakini kwa hali ilivyo hata kama zitahitajika Bilioni 2 tutazitafuta," DK Msolla aliliambia Mwanaspoti

"Tuna kazi kubwa ya kufanya ndani ya kikosi chetu, Hatuna ubora ambao tunastahili kuwa nao. Ubora wa kikosi tulichonacho haulingani na ukubwa wa jina la Yanga"

Viongozi wapya wa Yanga wameanza kazi kwa kishindo ambapo baada ya kuchaguliwa siku ya Jumapili, usiku huo huo walielekea mkoani Iringa kuiunga mkono timu ilipocheza na Lipuli Fc

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’