Siri ya Dk Msolla, Mwakalebela kupita kwa kishindo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 May 2019
Siri ya Dk Msolla, Mwakalebela kupita kwa kishindo

Wanachama wa Klabu ya Yanga wametaja sababu ya kuwachagua Dk. Mshindo Msolla na Fredrick Mwakalebela ni kuleta sura mpya ndani ya uongozi wa klabu yao.

Dk. Msolla na Mwakalebela walipata ushindi wa kishindo katika uchaguzi mkuu wa Yanga uliofanyika juzi kwenye Ukumbi wa Bwalo la Polisi, Oysterbay, jijini Dar es Salaam.

Dk. Msolla ambaye alishawahi kuwa kocha mkuu wa Taifa Stars alimshinda mpinzani wake wa pekee, Dk. Jonas Tiboroha, katika nafasi ya Mwenyekiti huku nafasi ya Makamu Mwenyekiti ikimuangukia aliyekuwa Katibu Mkuu wa zamani wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Mwakalebela.

Kaimu Mwenyekiti wa matawi ya Yanga Tanzania, Shaaban Mgonja, amesema Wanayanga wamepata kile walichokuwa wanahitaji.

Amesema kilio kikubwa cha wadau wa Yanga ilikuwa kupata sura mpya katika klabu ambazo zinauelewa wa mambo ya mpira wa kisasa ndani na nje ya nchi.

Mgonja alisema katika vikao vyao vingi walivyokaa na wanachama kabla ya uchaguzi huo, walikuwa wakitoa maoni ya viongozi wanaowahitaji na  sasa wamewapata.

“Tunashukuru kumaliza uchaguzi salama, hakika wanachama wa Yanga wametimiza malengo yao baada ya kupata viongozi tuliokuwa tunawahitaji," Mgonja aliliambia gazeti la Bingwa

“Tunaishukuru  Serikali na TFF kwa maelekezo yao na kutusimamia kwa ukaribu pamoja na changamoto zilizokuwepo.

“Kilichobaki kwa sasa ni sisi wenyewe kutoa ushirikiano kwa viongozi wetu ili kufikia ndoto itakayowezesha klabu ya Yanga kusimama tena,” alisema Mgonja.

Alifafanua kitu cha kwanza wanachohitaji kifanyike kabla ya yote, ni kuingia katika mfumo wa mabadiliko ili klabu kujiendesha kiuchumi na utawala bora.

Naye Mwenyekiti wa matawi Wilaya ya Ilala, Kondo Kipwata, alisema wanamfahamu Dk. Msolla kama injinia wa mpira na Mwakalebela mtu aliye na uzoefu katika soka hapa nchini.

“Tuna matumaini makubwa na viongozi tuliowachagua, Msolla ni injia wa mpira hakuna anayepinga, Mwakalebela amekaa TFF na aliyofanya yanajulikana, kinachotakiwa tuwape muda na wanachama wasiwe na haraka,” alisema.

Bingwa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
2h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
10h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’