Fedha zilizochangwa kuwekwa hadharani Mei 18

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 May 2019
Fedha zilizochangwa kuwekwa hadharani Mei 18

Mwenyekiti wa Kamati Maalum ya uhamasishaji Mh Anthony Mavunde amesema zoezi la michango litahitimishwa Mei 18 Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam wakati wa hafla maalum ya chakula cha usiku

Akizungumza juzi kwenye uchaguzi wa Yanga, Mavunde amesema siku hiyo wanatarajiwa kukusanya zaidi ya Mil 500 kutoka kwa wadau mbalimbali wa klabu hiyo

Aidha alisema pia watatangaza kiasi cha fedha zilizopatikana tangu zoezi hilo lililopanza chini ya Kamati yake

"Zoezi la michango limeanza muda mrefu na hamasa ni kubwa, hivyo Mei 18 katika hoteli ya Serena tutakuwa na hafla maalum kwa ajili ya michango kabla ya zoezi kufungwa na kukabidhi michango kwa uongozi"

"Tunawaomba Wanayanga waendelee kuchangia, Mei 18 tutaweka hadharani kiasi cha fedha zilizopatikana kabla ya kuukabidhi uongozi"

Hafla ya 'Gala Dinner' awali ilipangwa kufanyika Jumamosi ya Mei 11, hata hivyo iliahirishwa kufuatia kifo cha Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Dk Reginald Mengi ambaye alikuwa mdau wa Yanga

Hafla hiyo itafanyika wiki moja baada ya Wanayanga kumzika Dk Mengi anayetarajiwa kupumzishwa kwenye nyumba yake ya milele keshokutwa Alhamisi, Machame

Lakini habari njema ni kuwa lengo la kukiboresha kikosi cha Yanga kwa ajili ya msimu ujao litafanikiwa baada ya Mwenyekiti mpya wa timu hiyo Dk Mshindo Msolla kumuhakikishia kocha Mwinyi Zahera kuwa watampatia fedha zote alizohitaji kwa ajili ya usajili

"Bilioni moja na nusu aliyotaka Zahera kwa ajili ya usajili tutampatia. Hata akitaka fedha zaidi tutamuongeza," alisema Dk Msolla wakati akihitimisha kampeni juzi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
5h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
9h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
14h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
14h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’