Tumetolewa FA, tutaendelea kupambana kwenye ligi - Zahera

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 May 2019
Tumetolewa FA, tutaendelea kupambana kwenye ligi - Zahera

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema baada ya kupoteza mchezo wa nusu fainali kombe la FA kwa kufungwa mabao 2-0 na Lipuli Fc leo, wanahamishia nguvu zao kwenye ligi kuhakikisha wanashinda michezo minne iliyobaki

Zahera amesema licha ya kutofanikiwa kutinga fainali, msimu huu wamevuka malengo na matarajio ya awali

"Hakuna kitu kitabadilika juu ya mipango yetu, tunahitaji kushinda mechi nne zilizobakia ligi kuu," amesema Zahera

"Ukiangalia mpaka hapa tumefanikiwa kuliko matarajio. Mwaka huu tulianza ligi tukiomba mungu atusaidie japo tumalize nafasi ya sita au ya saba"

"Tulipaswa kumaliza nafasi ya sita au saba kutokana na changamoto tulizopitia msimu huu. Tulikubaliana tufanye nguvu tusimalize chini ya nafasi ya kumi"

"Mkiangalia tunaongoza ligi tokea mwanzo wa msimu mpaka leo. Malengo ya kutwaa ubingwa wa ligi na hata kombe la FA yalikuja baada ya kuona tumeweza kufanya vizuri licha ya changamoto zilizokuwa zinatukabili"

"Kazi waliyofanya wachezaji wangu ni nzuri sana. Tutaendelea kupambana kwenye ligi ili tuweze kushinda michezo yote minne iliyobaki"

Aidha akizungumzia mabadiliko aliyofanya kwenye kipindi cha pili amesema ilikuwa ni kazima kuwatoa Ajib na Mohammed Issa  na kuwaingiza Tambwe na Juma Abdul ili kwendana na aina ya uchezaji wa Lipuli Fc

"Lipuli walikuwa wengi katikati hivyo nililazimika kumuingiza Tambwe na Abdul ili kutumia mipira ya krosi kupitia pembeni kujaribu kusaka mabao ya kusawazisha"

"Mfumo huo ulitusaidia kwani tulipata karibu nafasi tatu za kuweza kufunga lakini tulikosa bahati"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
3h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
21h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’