Yanga kuikabili Lipuli Fc ikiwa na mzuka wa kutosha

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 May 2019
Yanga kuikabili Lipuli Fc ikiwa na mzuka wa kutosha

Yanga iko mkoani Iringa ambapo leo jioni itashuka uwanja wa Samora kuikabili Lipuli Fc katika mchezo wa nusu fainali kombe la FA (ASFC)

Habari njema kwa wachezaji wa Yanga ni kuwa leo watashuka dimbani wakiwa na sapoti ya viongozi wao wapya waliopatikana baada ya uchaguzi jana

Makamu Mwenyekiti Fredrick Mwakalebela anatarajiwa kuwepo uwanjani leo kuwaunga mkono wachezaji kuhakikisha wanashinda mchezo huo

Jana baada ya zoezi la uchaguzi kumalizika, Mwakalebela alisema ataondoka jijini Dar es salaam usiku huo kuwahi mchezo

"Mimi na wenzangu wachache tunaondoka usiku huu kuelekea Iringa kwenda kuwaunga mkono wachezaji wetu. Tunahitaji kushinda mchezo dhidi ya Lipuli ili tuingie fainali"

"Lengo letu ni kushiriki michuano ya kimataifa msimu ujao, tunahitaji kutwaa kombe la FA"

Aidha fedha taslim zaidi ya Mil 20 zilichangishwa na Wanachama wa Yanga jana ili kuipa motisha timu kuelekea mchezo huo

Yanga inahitaji kukomaa na kombe la FA ili kujihakikishia nafasi ya kushiriki michuano ya CAF msimu ujao

Β 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
16h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
21h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’