Dk Tiboroha akubali kushindwa, aahidi kumpa ushirikiano Dk Msolla

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 May 2019
Dk Tiboroha akubali kushindwa, aahidi kumpa ushirikiano Dk Msolla

Aliyekuwa mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Yanga Dk Jonas Tiboroha amesema baada ya Wanachama kumchagua Dk Msolla kuwa Mwenyekiti kwa kura nyingi, ni wakati wa kuvunja makundi na kushirikiana kuipeleka Yanga mbele

Dk Tiboroha amewashukuru wanachama 60 waliompigia kura na amewataka wavunje makundi na wamuunge mkono Dk Msolla

Ameahidi kushirikiana na Dk Msolla

"Napenda nitoe shukrani zangu kwa kamati ya uchaguzi, pili nawashukuru wapiga kura wote hakika wana Yanga mmeongea kwa sauti kubwa sana.

"Hatimaye tumempata Mwenyekiti, kama mgombea nampongeza sana mwenyekiti na pia namtakia kila la heri katika shughuli yake inayokuja

"Sio shughuli ndogo ila nina imani kubwa juu yake anaweza kutupeleka kwenye nchi ya ahadi.

"Lakini mimi kama mwana Yanga nilishamtumia ujumbe wa pongezi ndugu Mwenyekiti kwa kuwa nilishapata matokeo mapema kidogo

"Nimemwambia kabisa mimi kama mwana Yanga nipo tayari kumsaidia pale anapoona nafaa na kunihitaji

"Mwisho kabisa nawapongeza wale watu 60 walionipigia kura kwa maana kura zao zimewezesha kupatikana mshindi, ni muda sasa kuvunja kambi na utimu kuanzia sasa wote ni timu Msolla, Ahsanteni sana"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
12h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
16h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
17h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
21h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
21h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’