Cannavaro kuugeukia ukocha

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
11 Sep 2017
Cannavaro kuugeukia ukocha
Nahodha wa Yanga Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amesema atakapostaafu kucheza soka anataka kusomea ukocha ili kuja kuchukua mikoba ya kocha wake wa sasa George Lwandamina.

Cannavaro amekuwa hapati nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza kutokana na umri wake kumtupa mkono.

“Hata kama sichezi lakini nafurahi kuwa benchi kwasababu najifunza mambo mengi kutoka kwa makocha waliopo na lengo langu baada ya kustaafu kucheza nataka kuja kuifundisha Yanga siku zijazo,” amesema Cannavaro.

Nahodha huyo ameuambia mtandao wa Goal, hakuna kinachoshindikana katika hilo kwani kwakipindi cha misimu 11, alichoitumikia Yanga ameweza kujifundisha mambo mengi kutoka kwa makocha mbalimbali ambao wamepitia timu hiyo.

Mkongwe huyo amesema mipango yake baada ya kustaafu kucheza soka ni kwenda kusomea ukocha ili kuongeza elimu ambayo itamfanya kuwa na vigezo vya kuweza kufundisha timu za Ligi Kuu hasa Yanga.

Cannavaro alijiunga na Yanga mwaka 2006, akitokea Tembo ya Zanzibar akiwa na wenzake watatu ambao ni kipa Mbarouk Selemani Mohamed Mkweche na Thomas Morice.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
2h ago
READ MORE →
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
7h ago
READ MORE →
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
11h ago
READ MORE →
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
12h ago
READ MORE →
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
12h ago
READ MORE →
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
13h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
17h ago
READ MORE →
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE →
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE →
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE →