Igangula kuanza na uwanja wa Kaunda

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 May 2019
Igangula kuanza na uwanja wa Kaunda

Mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Baraka Igangula amesema kama atachaguliwa kuwa Mwenyekiti wa klabu hiyo, atahitaji miezi mitatu tu kukamilisha ukarabati wa uwanja wa Kaunda ambao unamilikiwa na Yanga

Aidha Igangula anayechuana na Dk Mshindo Msolla, Dr Jonas Tiboroha na Elias Mwanjala kuwania uwenyekiti wa Yanga, amesema kutokana na uzoefu mkubwa aliyokuwa nao kwenye uongozi wa Yanga, ana lengo la kuifanyia timu hiyo mambo makubwa na kamwe hataweka mbele maslahi binafsi

"Tutakuwa na mpango wa muda mfupi ambao tutaukarabati uwanja wetu pale klabuni, huku tukiwa na mpango wa muda mrefu wa kujenga uwanja nje ya mji, hata ikiwezekana Kibaha, Pwani ambao utakuwa na hosteli, maduka na ofisi mbalimbali," amesema Igangula

Igangula pia ameunga mkono mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa Yanga akiahidi kulikamilisha zoezi hilo haraka

"Nitasimamia mchakato wa mabadiliko na kuhakikisha unakamiliki punde tu nitakapoingia madarakani. Nitaajiri wataalamu wenye ujuzi wa masuala ya kampuni ili tuachane na utaratibu huu wa kuendesha klabu kwa mazoea"

Ahadi nyingine alizotoa Igangula ni kuanzisha bima ya afya itakayowalenga wanachama, saccos, vicoba na mfuko wa kufa na kuzikana, kama sehemu ya kuimarisha umoja, upendo na mshikamano baina ya wanachama na viongozi wa Yanga

Pia atahakikisha wachezaji na benchi la ufundi wanalipwa mishahara kwa wakati, kusimamia mikataba na mapato ili kudhibiti ufisadi

Uchaguzi wa Yanga utafanyika Jumapili, May 05 ukumbi wa bwalo la Polisi, Osterbay jijini Dar es salaam

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
6m ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
5h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
20h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’