Amissi Tambwe atatibu safu ya ushambuliaji Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Sep 2017
Amissi Tambwe atatibu safu ya ushambuliaji Yanga
Sifa moja kubwa ya Amissi Tambwe ni umahiri wake wa kuvizia kufunga mabao langoni kwa timu pinzani.

Wakati mwingine unaweza ukadhani hayupo uwanjani lakini ukiona nyavu za timu pinzani zinatikisika usishangae kumuona anashangilia.

Huyu ndiye mchezaji pekee anayekosekana kwenye safu ya ushambuliaji ya Yanga. Hata hivyo, habari njema ni kwamba upo uwezekano mkubwa atakuwa tayari kucheza kwenye mchezo dhidi ya Ndanda Septemba 23 kwenye dimba la Uhuru.

Tambwe akirejea naamini safu ya ushambuliaji ya Yanga itakaa sawa.

Kwa sasa Yanga imelazimika kumtumia Donald Ngoma kama straika kutokana na ukweli kwamba hakuna mchezaji mwingine anayeweza kumudu nafasi hiyo zaidi yake.

Lakini Ngoma anafaa zaidi acheze namba 10, awe nyuma ya mshambuliaji wa mwisho.

Obrey Chirwa nae ni mzuri zaidi anaposhambulia akitokea pembeni. Haitakuwa vibaya kama kocha George Lwandamina akajaribu kumtumia kama winga sambamba na Ajib.

Dalili zinaonekana msimu huu mikoani kutakuwa kugumu sana kuchukua alama zote tatu lakini sasa inabidi kocha na benchi lake la ufundi wahakikishe michezo yote itakayopigwa kwenye dimba la Uhuru Yanga inachukua alama zote tatu.

Na hili litafanikiwa kama safu ya ushambuliaji itafanya kazi yeke ya kupachika mabao ipasavyo. Safu ya ulinzi ya Yanga imeimarika sana tangu kuwasili kwa kiungo Papi Kabamba Tshishimbi.

Tshishimbi ndiye mlinzi wa safu ya ulinzi ya Yanga. Huyu mtu ni habari nyingine, anaifahamu hasa kazi yake. Amekuwa akishirikiana vyema na walinzi wa kati Dante na Yondani.

Kipa Youthe Rostand naye ameifanya Yanga kuwa imara zaidi kwenye ulinzi. Anazungumza na mabeki wake na ni mkali pale wanapofanya makosa.

Ndio, makosa ya hapa na pale hayakosekani lakini lazima tukiri safu ya ulinzi ya Yanga ndiyo imekuwa ikiibeba timu tangu pambano la Ngao ya Jamii dhidi ya Simba.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’