Dk Msolla azindua kampeni Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 May 2019
Dk Msolla azindua kampeni Yanga

Mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti katika uchaguzi wa Yanga utakaofanyika May 05, Dk Mshindo Msolla amezindua kampeni zake leo Makao Makuu ya klabu ya Yanga, jijini Dar es salaam

Dk Msolla ambaye kitaalamu ni Mwalimu wa mpira wa miguu (kocha) aliyewahi kuinoa Taifa Stars, ametaja vipaumbele vyake ambavyo atavitekeleza kama atachaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Yanga

Baadhi ya vipaumbele hivyo ni pamoja na Kujenga umoja na ushirikiano, Kuendeleza mchakato wa mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji, Kuendeleza miradi yote ya klabu iliyopo pia kuanzisha mipya, Kuweka na kusimamia misingi ya utawala bora pia kuweka misingi ya Yanga kuwa na timu imara

Dk Msolla amesema anataka kuona ushirikiano baina ya timu na mashabiki na wanachama wake unaimarika zaidi na ameunga mkono zoezi la kuichangia Yanga linaloendeshwa

"Nataka kujenga umoja ndani ya klabu kwa maana ya kuirudisha timu kwa wanachi hivyo sio vibaya wenye timu kuichangia klabu yao"

Aidha DK Msolla amesema atabadili mfumo wa uchaguzi wa Yanga unaotoa fursa pekee kwa wanachama wa Dar es salaam kushiriki michakato ya uchaguzi

"Natambua kuwa wanachama wengi wa Yanga ambao hushiriki uchaguzi ni wale ambao wapo Dar, ndani ya uongozi wangu kama nikipewa nafasi basi wa mkoani nao watapata haki hiyo.

"Tutakuwa na mfumo ambao utawawezesha kupiga kura wakiwa kwenye matawi yao"

Kuhusu utawala bora Dk Msolla amesema uongozi wake hautaingilia majukumu ya kocha Mwinyi Zahera

Amesema kocha huyo ni mtu muhimu kwa klabu ya Yanga, ni bahati kuwa nae hasa ikizingatiwa timu inapita katika kipindi kigumu sana

"Mimi ni kocha wengi wananifahamu, akihitaji ushauri wa kiufundi nitampatia lakini nitaingia Yanga kama mwenyekiti hivyo niseme wazi kuwa nitamwacha awe huru kutekeleza majukumu yake.

"Uongozi wangu hautakuwa na mipango ya kuachana naye, mara kadhaa nimekuwa nikisema wazi kuwa Yanga tunabahati ya kupata kocha wa namna hii"

Pia Dk Msolla amesema atahakikisha Yanga inakuwa na misingi mizuri ya kuendeleza vijana wa kikosi B kwa lengo la kuja kuwatumia kikosi cha kwanza

Wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi Yanga wameendelea kuzindua kampeni ambazo zitadumu hadi Jumamosi, May 04 siku moja kabla ya uchaguzi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
17h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
21h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
22h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
22h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
2d ago
READ MORE β†’