Sevilla kucheza na Simba May 23, sababu yatajwa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 Apr 2019
Sevilla kucheza na Simba May 23, sababu yatajwa

Kampuni ya SportPesa ambao ndio wadhamini wa timu za Yanga na Simba, wameitangaza klabu ya Simba kuwa ndio itakayocheza na Sevilla mchezo wa kirafiki utakaopigwa May 23 katika uwanja wa Taifa

Akitangaza uamuzi wa kuichagua Simba, Katibu Mkuu wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF), Wilfred Kidao amesema wameangalia mafanikio ya Yanga, Simba na timu nyingine za Tanzania kwenye michuano ya SportPesa iliyofanyika nchini hivi karibuni

"Ni wazi, Simba ndio klabu iliyofika hatua ya nusu fainali katika michuano ya SportPesa, hivyo tumeona ni vyema wakatuwakilisha katika mchezo huo wa Kimataifa," amesema

Awali kulikuwa na mkanganyiko wa timu ipi kati ya Yanga au Simba ipewe nafasi ya kucheza na Sevilla hali iliyopelekea kutolewa hoja ya kuzipambanisha timu hizo ili mshindi apate fursa hiyo

Mkurugenzi wa Utawala na Uzalishaji wa Sportpesa Tanzania, Tarimba Abasi amesema, mchezo huo utakuwa chachu ya maendeleo ya soka la Tanzania na utatangaza ukubwa wa soka la Tanzania katika nchi mbalimbali

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
5h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
10h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
10h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
20h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’