Ngoma, Chirwa warudi kuiwinda Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Apr 2019
Ngoma, Chirwa warudi kuiwinda Yanga

Washambuliaji Donald Ngoma na Obrey Chirwa kesho wanatarajiwa kuiongoza safu ya ushambuliaji ya Azam Fc mchezo dhidi ya Yanga ambao utapigwa uwanja wa Uhuru

Wachezaji hao walijiunga na Azam Fc msimu huu wakitokea Yanga kwa nyakati tofauti

Ngoma ndiye aliyekuwa wa kwanza kutua Azam Fc mwanzoni mwa msimu akiwa mchezaji huru baada ya Yanga kufikia makubaliano nae ya kuvunja mkataba wake

Majeraha ya muda mrefu yalisababisha Yanga kuamua kuachana na mshambuliaji huyo aliyeipa mafanikio kwenye misimu yake miwili ya kwanza

Hata hivyo Azam Fc ililazimika kusubiri kwa karibu wiki 10 kupata huduma ya mshambuliaji huyo raia wa Zimbabwe.

Azam ilimpeleka Afrika Kusini ili kupata matibabu zaidi

Uvumilivu wao umekuwa na faida kwao kwani Ngoma amerejea kwenye kiwango chake mpaka sasa akiwa ameifungia Azam mabao 10 kwenye ligi

Chirwa alitua Azam wakati wa usajili wa dirisha dogo akitokea nchini Misri ambako alivunja mkataba na timu ya daraja la pili aliyokuwa akiichezea

Aliondoka Yanga mwishoni mwa msimu uliopita baada ya mkataba wake kumalizika

Wawili hao ndio wachezaji wa kuangaliwa zaidi na safu ya ulinzi ya Yanga

Dante hawahofii

Beki Andrew Vicent Chikupe maarufu kama Dante amesema hana hofu ya kuwakabili washambuliaji hao kwani anawafahamu vizuri

"Ngoma na Chirwa tunawafahamu, tumecheza nao kwa muda mrefu hivyo hawatatusumbua," amesema

Chikupe anategemewa kuongoza safu ya ulinzi ya Yanga kesho ambayo itamkosa mkongwe Kelvin Yondani aliyefungiwa michezo mitatu

Beki Abdallah Shaibu 'Ninja' anatarajiwa kucheza sambamba na Chikupe katika safu ya ulinzi ya kati

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’